Beki wa Liverpool Dejan Lovren amemshutumu mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku kwa kumpiga teke usoni kwa makusudi katika mechi ya Jumamosi.
Wawili hao walihusika katika mgogoro wa muda mfupi kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza katika mechi iliotoka sare ya 0-0 katika uwanja wa Anfield, huku Lovren akisalia amejibiringisha katika uwanja akishikilia uso wake kwa uchungu mwingi.
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alisema kuwa alidhani kwamba Lukaku alihitaji kupewa kadi nyekundu , lakini hakuna hatua yoyote iliochukuliwa.
''Ukweli ni kwamba alifanya alichokifanya kwa makusudi'', alisema Lovren.''Alikuwa juu yangu na angeondoka tu''.
''Kawaida akifanya hivyo yeye huomba msamaha , lakini nilimuona akiwa amekasirika wakati wa mechi kwa hivyo pengine hiyo ilikuwa sababu''.
Alipoulizwa iwapo hakufurahia kwamba mshambuliaji huyo wa Ubelgiji hatopewa adhabu yoyote , Lovren alijibu.''Huo sio uamuzi wangusiwezi kusema sikufurahia lakini hivyo ndivyo ilivyo''.
Post a Comment