0

Moto uliochomwa Pembezoni mwa Barabara waripotiwa kusababisha ajali mbaya ya gari, Ajali hiyo imetokea katika Eneo la kijiji cha Mihambwe – Mchinga katika halmashauri ya Wilaya ya Lindi.
Taarifa za awali zinasema kuwa madereva wa ma lori hayo mawili wamefariki dunia papo hapo na tingo Mmoja huku majeruhi 3 wamewahishwa Hospitali ya Mkoa Sokoine kwa Matibabu. MaLori hayo moja ikiwa mali ya Dangote Cement na jingine likiwa mali ya Twiga Cement.
Sababu ya Ajalihiyo inasemwa kuwa ni moto uliowashwa pembeni mwa barabara na kusababisha moshi mnene barabarani na kufanya madereva hao kushindwa kuona mbele.

Post a Comment

 
Top