0


Timu ya Hawili fc Vs New Vision fc ni mchezo wa nusu fainali ligi ya alizeti katika mchezo huo uliochezwa oktoba 23 timu ya Hawili fc iliibuka na ushindi wa goli 1-0 goli hilo lilifungwa na Imani Mbesigwe dakika ya 82 mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale inayoendelea  mkoani Lindi.

Kwa ushindi huo timu ya Hawili fc ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la alizeti cup 2016 sasa watakutana na timu ya Leopard fc kwenye mchezo wa fainali siku ya ijumaa oktoba 27 mchezo huo utachezwa uwanja wa wilaya ya Liwale.

Timu ya Super stars itacheza na New Vision fc ili kumpata mshindi wa tatu

Post a Comment

 
Top