0

Baadhi wanasema walifikia hatua ya kuzihama nchi zao kwa ushawishi tu
Baadhi wanasema walifikia hatua ya kuzihama nchi zao kwa ushawishi tu
BBC imepata nafasi adimu ya kuingia katika kambi kubwa inayowazuia wakimbizi nchini Libya, na kukuta wakiwa katika hali mbaya.
Wanaoshikiliwa wanasema wamejazwa katika vyumba mpaka kufikia hatua ya kulala wakiwa wamesimama.
Hawana huduma muhimu kama maliwato,huku chakula kikiwa ni cha shida.
  Chumba hiki kinahifadhi watu wengi kushinda uwezo wake
Chumba hiki kinahifadhi watu wengi kushinda uwezo wake
Wengi wao walirubuniwa na wanaofanya biashara za kusafirisha watu na wamekwama kuingia Ulaya.
Msimamizi wa eneo hilo anasema wanahitaji misaada ya kibinaadam kuweza kuwasaidia.

Post a Comment

Top