0

 VIJANA  WALIOHITIMU  MAFUNZO YA  MRADI  WA UWEZESHAJI  VIJAN  KIUCHUMI (YEE)
VIONGOZI  KWENYE  MAHAFALI YA  MRADI  WA  UWEZESHAJI  VIJANA   KIUCHUMI
Na Mwandishi wetu
Vijana 264 kutoka  kata   za  Mwenge,  Jamuhuri  ,Msinjahili ,Raha  leo, Rasbura na  Mbanja  katika  Manispaa  ya  LINDI  wametunukiwa vyeti  vyao  baada  ya  kuhitimu  mafunzo  ya  fani  mbalimbali  kupitia  mradi  wa  uwezeshaji  vijana  kiuchumi.

Mkuu  wa  chuo  Veta Lindi  Samuel  Ng’andu alisema mradi unafadhiliwa  na  jumuiya  ya  ulaya  na kutekelezwa  na  Mashirika  ya  plan International Tanzania  kwa  kushirikiana  na  mamlaka  ya  mafunzo  ya  ufundi  stadi  VETA na  shirika  na  VSO ,CODERT, UHIKI  na  Jamii.
Alisema lengo  la  mradi  ni  kuongeza wigo wa  mafunzo  ya ufundi  stadi  ili kuwafikia  walengwa wengi kwa kuunga  juhudi  za  serikali  za kuwapatia  ajira  vijana  9100  wa   mikoa  Pwani,Morogoro,Lindi,Mtwara.

Ng’andu Alisema Manispa  ya   Lindi  vijana 500 watanufaika  kutoka  kata  9 za mikumbi,Mitandi Mwenge Msinjahili,  Jamuhuri, Mbanja, Mlandege , Makonde, Mladege na  Rasbura  wakati  Halmashauri ya  wilaya  Lindi  vijana 1000 watanufaika  na  mpango  kutoka  kutoka  kata 9  za  Nyangao ,  Majengo, Nyengedi, Mtua , Mtama, Kiwalala, Kitomanga, Mchinga, Kilangala, na  Milola.

Alisema  mradi unawalenga  vijana  wenye  umri wa  miaka 15  hadi 35 ambapo  asilimia 53 ni  wasichana  na  asilimia 47  ni  wavulana niongoni  mwao  vijana  wenye  ulemavu asilimia  10 na  wahitimu  watakao  patiwa  vyeti  ni  vijana  264  wakiume  136 na  wakike 128,  na walemavu  watatu, wakiume 2 na moja  wa  kike.

Post a Comment

 
Top