
Manchester City ime
uraruwa ulinzi hafifu wa Liverpool na kunyakua ushindi mkubwa dhidi ya
wageni wake wa kikosi cha wachezaji 10 Liverpool, na kufanikiwa kukwea
kwenye orodha ya ligi.
Sergio Aguero alifungua mvua ya mikwaju kwa kumchenga kipa wa Liverpool Simon Mignolet.
Sadio Mane alitolewa uwanjani baada ya kunyanyua mguu wake uliomgonga kipa wa City, Ederson, aliyetibiwa uwanjani kwa dakika 10.
Gabriel Jesus aliongeza jingine na Leroy Sane kumalizia kwa mawili ya mwisho na kukamilisha ushindi wa 5-0.
Kevin
de Bruyne alitoa pasi safi kwa goli la ufunguzi la Aguero na pia
alimtambua na kumpa pasi Jesus aliyekuwa wazi na kufanikiwa kuifungia
City katika muda wa ziada baada ya kujeruhiwa kwa Ederson.
Ushindi
huu unakiinusha kikosi cha Pep Guardiola juu ya mahasimu Manchester
United kwenye ligi, wanaokuwa wageni wa Stoke baadaye Jumamosi.
Na unahakikisha kushindwa kwa mara ya kwanza katika msimu kwa kikosi cha Jurgen Klopp.
Post a Comment