0



Klabu ya Simba, Jumatatu Septemba 4 imeitangaza Kamati Maalum itakayohusika na kumtafuta mzabuni ambaye atanunua hisa 50% za timu hiyo katika suala lake la uendeshaji mpya wa klabu hiyo.


Kamati hiyo itaundwa na wajumbe watano na itaongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo sambamba na wajumbe wanne ambao ni Wakili Damas Ndumbaro, Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu, Yussuf Majjid Nassor na Abdulrazak Badru ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ua Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania.

Kamati itakutana Alhamisi wiki hii kuanza kazi ya kuwajadili wanachama ambao watataka kuzinunua hisa hizo ambapo watafuata sheria za manunuzi ya umma ambapo watakaa kwa siku 45 kabla ya kumtangaza mzabuni wa timu hiyo.

Post a Comment

 
Top