0

Boma hili ni kati ya maboma machache ya wajeruman na ambayo yapo katika Hali mbaya zaidi kiuhifadhi kwa sababu hata halmashaur yetu haijajuwa ianzie wapi. Na Katika dunia ya leo rasilimali kama hii haitakiwi iendeshwe kwa kodi za wananchi, inatakiwa ijiendeshe yenyewe kupitia viingilio na 'tips' za watalii. 

Boma hili limebeba historia kubwa ya watu wa Liwale na maisha yao wakati wa ukoloni. Bahati mbaya tumekosa 'full time story tellers/tour guides' . Kwa sababu kitaalam kivutio cha utalii wa kitamaduni kikikosa maelezo kinageuka uchafu. Hivyo wasimualiaji hawa kuwepo kwao kunaleta maana sahihi ya jengo lile na umuhimu wake katika Tanzania ya leo.

MAANA YA UTALII
Kwa mujibu wa sera ya utalii ya Tanzania ya mwaka 1999 inautafsiri utalii kama kitendo cha mtu/binadam kusafiri kwenda nje ya eneo analoishi kwa muda usiozidi mwaka kwa lengo la kufanya shughuli ambayo haimuingizii kipato (URT 1999).


Sheria ya utalii ya mwaka 2008 imeutafsiri utalii kama ni kitendo cha mtu kusafiri kwenda nje ya eneo analoishi kwa zaidi ya masaa 24 na isiyoZidi mwaka moja na lengo kuu la safari hiyo ni kufanya shughuli ambayo si ya kuongeza kipato; na ikiwa kitendo hicho kitafanywa na mtanzania ndani ya Tanzania kitaitwa utalii wa ndani (URT 2008).

Kwa taafsiri ya miongozo yetu ya nchi utalii ni kusafiri nje ya makazi yako, pia ni kwenda kufanya shughuli ambayo lengo lake si kuingiza kipato na mwisho ni lazima iwe zaidi ya siku na isizidi mwaka.

kwa ufupi utalii kama shughuli inayohusisha kustarehe kuna vitu vitatu vya msingi ambavyo vikikosekana mantiki mzima ya utalii inakuwa haipo tena navyo ni Kivutio/vivutio (Attractions), njia za kuvufikia vivutio (Accessibility) na huduma za msingi (Amenities) kama vile huduma za Malazi, maduka, vituo vya afya na kadhalika. Hizi wataalam wa masuala ya utalii wanaziita 'three As'. Na ukweli ni kwamba kikikosekana kimoja Kati ya hivyo inakuwa hamna utalii labda iwe kitu kingine. Na kwa kuzingatia tafsiri zilizoelezwa hapo juu, endapo mtu akatoka na ndege akaja Liwale na akatembelea kivutio kimoja wapo na akapanda ndege tena na kurudi alikotoka siku hiyo hiyo huo hautakuwa utalii. Utalii unamtaka mtu huyo atumie angalau siku moja kwenye eneo ambalo kivutio kinapatikana.


BAADHI YA VIVUTIO VYA UTALII WILAYAN LIWALE
Eneo la Jumuiya ya hifadhi ya Wanyamapori Magingo.
Kama tunavyofaham wanyamapori ni rasilimali muhimu sana katika sekta ya utalii. Shughuli mbili kubwa ambazo zinaongeza idadi ya watalii kupitia wanyamapori ni utalii wa kuangalia wanyama wakubwa (Game viewing) pamoja na ule utalii wa kuwinda ( Tourist Hunting). 


Jumuiya Magingo imeanzishwa mwaka 2003 na vijiji nane vyote vya wilayan Liwale ambavyo ni Ndapata, Mpigamiti, Mlembwe, Barikiwa, Chimbuko, Mirui, Naujombo na kimambi kwa mujibu wa mpango wa usimamizi wa kanda wa Jumuiya (2004 - 2009) Magingo ina kanda tatu za Uwindaji wa kitalii, kanda moja ya uwindaji wa kienyeji na moja ya utalii wa picha ( utalii wa kuangalia wanyama). 

Hivyo hiki ni kivutio Kimoja Kikubwa cha utalii kwa kuzingatia kwamba eneo Lina idadi kubwa ya wanyamapori na linatoa mchango mkubwa katika kuimarisha ubora wa mfumo wa kiikolojioa wa selous na Mikumi (selous-mikumi ecosystem). 


Lakin pia Jumuiya imepakana na Mbuga kubwa kuliko zote hapa nchini ya selous (kwa taarifa yako mbuga ya selous ni aslimia tano 5% ya eneo lote la Tanzania bara) fursa hii inaipa Jumuiya kipaumbele katika uhifadhi ambapo wanyamapori wote wanaopatikana katika mbuga ya selous wanapatikana Magingo kasoro twiga kutokana na sababu za kiikolojia. Kwa sasa utalii unaofanyika katika eneo hili ni uwindaji wa kitalii pekee. Tutaeleza sababu huko mbele.
KWA LEO NAOMBA NIISHIE HAPA ILA INAENDELEA  UNGANA NASI KWA USHAURI NA MAONI 




Itaendelea wiki ijayo...................


Tafadhali usisite kutoa maoni yako
Makala hii Imeandaliwa na; 

Mohamed Kamuna & Mwandae Mchungulike 


          mmchungulike@gmail.com au liwalemedia@gmail.com

Post a Comment

 
Top