boma la zamani lilipo wilayani Liwale
Tarehe 12 July ya mwaka
1975 liwale ilitangazwa na
kuzinduliwa rasmi kuwa wilaya na
halimashauri moja wapo ya
mkoani lindi.kabla, ilikuwa ni
sehemu tu ya kiutawala ya wilaya
ya Nachingwea.
Wilaya ya Liwale ni miungoni mwa
wilaya kongwe hapa Tanzania
kwani ni baada ya miaka 14 tu ya
uhuru wa Tanganyika Desemba 9,
1961na baada ya miaka 11 tu ya
muungano wetu wa Tanganyika na
Zanzibar pale April 26, 1964 ndipo
Liwale ilipata hadhi hiyo ya kuwa
wilaya.
Namo tarehe 12 july 2017 wilaya
yetu inatimiza miaka 42! Kama
ingekuwa ni mtu basi tungesema
wilaya yetu imekidhi sifa ya umri
wa kuania urais kwa mujibu wa
katiba yetu ya JMT. Ndani ya
miaka 42 ya kuishi kama wilaya
yaliotokea ni mengi kwenye wilaya
yetu,natamani leo ningekua
naandika kuhusu maendeleo ndani
ya hiyo miaka 40! lakini kwa
bahati mbaya leo sina lesso, lesso
yangu ya kujifutia machozi na
kamasi nimeifua, hivyo sitagusa
huko badala yake, hebu leo
tujikumbushe Mabadiliko ya
maeneo ya taasisi mbalimbali za
serikali kwa kipindi hiki cha miaka
42.
Je, unaijua mitaa maarufu enzi
hizo? Unajua ilipokua hospitali
zamani kabla kuhamishiwa ilipo
sasa?. Polisi na benki je? Karibu
tusafiri wote!
1) Miaka ya 60 na hadi mwishoni
mwa miaka ya 70, mitaa iliyokuwa
maarufu ni miwili nayo ni
Makonjiganga na Likongowele.
Lakini makonjiganga ndio ulikuwa
hasa Mtaa wenye pilika pilika
nyingi. Pilika hizo na umaarufu
wake ulichagizwa na uwepo wa
taasisi mbalimbali kama vile benki,
hospitali ,polisi na uwepo wa
boma ya wajerumani ambayo
ilikua inatumika kuratibu shughuli
za kiutawala kabla ya kugeuzwa
kuwa kituo cha polisi. Miungoni
mwa koo marufu za wakati huo
kwenye mitaa hiyo ni Kichombaki,
Nganola,Mmango,
Ngamange,Mkwawa,kimamba na
Mahamudu.
2)Hospitali
Kabla ya kujengwa hopitali eneo
ilipo sasa, miaka ya 60 hadi miaka
70 mwishoni hospitali ilikua eneo
linalojulikana kama "miduleni" ni
pale ilipo shule ya awali ya
montasory(?).Ndipo huduma za
Afya zilipo kuwa zinatolewa.
3) Jengo la utawala
Boma lile la wajerumani kwa mda
mrefu lilitumika kama jengo la
utawala. Shughuri nyingi za
kiserikali na hasa zile za kiutawala
zilikuwa zikifanyikia hapo. Baadae
shughuli hizo za kiutawala
zilihamishiwa pale zilipo sasa.
Ukiwa Liwale si ajabu kumsikia
mkazi wa hapa na haswa kwa wale
wazee "naenda bomani"wakiwa
wanamanisha wanakwenda
kwenye ofisi hizo za halimashauri
ya wilaya. Makosa hayo hujitokeza
kwa sababu tu ya mazoea ya
kihistoria kuhusisha na lile boma
la wajerumani.
4)Polisi ya zamani
Polisi kabla ya kuwa kwenye kituo
wanachokitumia sasa, walikuwa
wakilitumia boma la wajerumani
kama kituo cha polisi.
5)Benki ya zamani "Green house"
Jengo la kituo cha polisi
linalotumika sasa ndipo ilipokuwa
benki ya serikali na kipindi hicho
jengo hili lilitambulika kwa jina
maarufu la"Green house".ndio
lilikuwa jengo rafiki kwa wafanya
kazi kila mwisho wa mwezi.
6)Ilipo TRA liwale leo ndipo
lilipokuwa jengo na duka maarufu
la ushirika "KABAMBE"(?)
Hivyo ndivyo baadhi ya mambo
yalivyokuwa na mabadiliko yake
kwenye maeneo na majengo ya
taasisi mbalimbali wilayani Liwale.
Itaendelea endelea kuwa nasi ili ujue mengi zaidi........
kiwanda cha kutengeneza mafuta ya alizeti cha chama cha ushirika umoja amcos kilichopo wilaya Liwale mkoani Lindi.
wanachama zaidi ya 770 wa chama cha ushirika umoja amcos kilichopo wilaya Liwale mkoani Lindi.
Wanachama wa chama cha ushirika cha msingi Umoja zaidi ya 770 walioudhulia mkutano mkuu wa chama uliofanyika katika ghala mkuu la chama hicho mei 15 mwaka 2017
Post a Comment