Serikali ya Sierra Leone imesema kwa zaidi ya watu 500 wamethibitika kufariki baada ya mmomonyoko mkubwa wa udongo kutokea wiki iliyopita katika mji mkuu Freetown.
Wengine zaidi ya 800 hawajulikani walipo, ikisemekana kwamba wamefukiwa katika udongo huo.
Kamati ya dharura nchini humo imesema kwamba zaidi ya watu elfu sita wameathiriwa na janga hilo.
Mmomonyoko huo mkubwa wa udongo ulitokea baada ya mvua kubwa kunyesha, ambapo nyumba nyingi zilikuwa chini ya milima.
Post a Comment