Mchezaji wa timu ya Mitumba fc akimiriki mpira kwenye mchezo wa augosti 14 dhidi ya Storaway fc katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Golikipa wa timu ya Storaway akijishikia kiuno alikuwa amini kilichitokea kwenye mchezo huo kufungwa magoli 3-0
Michuano ya Ligi ya Kazumari cup inaendelea kutimua vumbi katika hatua ya makundi jana augosti 14 kulikuwa na mchezo wa watani wa jadi kati ya Mitumba fc dhidi ya Storaway fc mchezo ulipigwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Mchezo huo ulikuwa aina yake na ulikuwa na mvuto kwa mashabiki wa soka ikiwa timu ya Storaway fc ikiwa na historia ya kutokufungwa lakini rekodi hiyo jana ilifutwa baada ya kukubali kichapo cha magaoli 3-0.
Magoli ya mitumba fc yalipatika mapema namo dakika ya 3 likifungwa na Haikosi Mpwate,Saidi Matumla dakika ya 26 na goli la tatu kifungwa na Haikosi Mpwate dakika ya 28.
Katika kipindi cha pili hakuna timu iliyoweza kufumania nyavu za mwezake licho ya mchezo huo kipindi cha pili kusimama kutokana na baada ya mashabiki wa timu wa Storaway fc kumtishia kibendela kutotimiza majukumu yake.
Kapteni wa timu ya Mitumba fc,Haikosi Mpwate alisema mchezo dhidi ya wapizani wao ulikuwa wa upizani sana lakini waliwazidi mbinu za kimchezo na nafasi walizopata waliweza kuzitumia vema na kufanyikiwa kuibuka na ushindi mnono.
Leo augosti 15 kutakuwa na mchezo wa mwisho mmoja katika hatua ya makundi watashuka dimbani Mifugo fc dhidi ya New generation baada ya mchezo huu kutakuwa na hatua ya robo fainali na nusu failina na augosti 25 kutakuwa na fainali.
Post a Comment