Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Nachingwea Ahmadi Makoroganya kulia akiwa kwenye kikao , kushoto, mkurugenzi wa wilaya Kilwa Zablon Bugingo
Jumla ya shilingi milioni 219 .00 Zimetengwa na Halmashauri ya ya wiaya Nachingwea kwa ajili ya ukarabati wa soko na maegesho ya magari stand ya mabasi.
Ahmad Makoroganya,mwenyekiti wa Halmshauri hiyo alisema kwa kutambua umuhimu wa soko kuu h kwa wakazi wananchi wa wilaya ya Nachingwea na nje ya wilaya hiyo ,Halmashauri imetenga shilingi 135.00 milioni kwa ajili ya kulifanyia ukarabati na shilingi 18.00 milioni kwa ajili ya soko dogo la Voda.
Makoroganya alisema ujenzi wa kituo kipya cha mabasi upo katika hatua za mwisho kukamilika.Ambapo hivi sasa bado kukamilisha ujenzi wa maegesho tu.Huku akibainisha kuwa Nazi hiyo imetengewa shilingi 66.00 milioni na halmashauri imeendelea kupeleka fedha kwenye vikundi vya ujasiriamali vya wanawake na vijana vikundi 34 vya wanawake na 24 vya vijana vimepewa mikopo.
Post a Comment