Marekani imeyawekea vikwazo makampuni kadhaa ya Urusi na China,kutokana na madai kuwa mataifa hayo mawili yanaisaidia Korea Kaskazini katika mpango wake silaha za Nyukilia.
Mapema mwezi huu,wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa walipiga kura kupitia uwekwaji vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.
Hata hivyo ofisi ya mambo ya nje ya Marekani inayohusika na udhibiti wa mali, imetangaza vikwazo dhidi ya makampuni kumi kutoka nchini China na Urusi na makampuni mengine binafsi sita.
Vikwazo vya kiuchumi vinatarajiwa kuendelea kama hatua ya kuishinikiza Korea Kaskazini na washirika wake kuachana na uendelezaji mpango wa silaha hizo za nyukilia.
China imeijibu Marekani kwa kusema kuwa inapaswa kusahihisha mara moja kosa hilo la kuyaadhibu makampuni ya China.
Naye waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema kuwa anaamini ufumbuzi kati ya Marekani na Korea Kaskazini unaweza kupatikana kupitia mazungumzo.
Tillerson ameipongeza Korea Kaskazini kwa kuonyesha hali ya utulivu kwa majumaa kadhaa yaliyopita ambapo haijafanya majaribio mengine ya makombora yake tangia baraza la usalama la umoja wa mataifa lilipopitisha vikwazo dhidi ya taifa hilo.
Post a Comment