0
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
VYAMA vya msingi vya ushirika nchini (AMCOS) vimekumbushwa wajibu wake wakutenga fedha kwenye bajeti zake kwa ajili ya mafunzo yatakayowajengea uwezo wa kiongozi na utendaji viongozi na watendaji wake.
Wito huo umetolewa leo na kaimu mrajisi wa tume ya maendeleo ya ushirika, Charles Malunde, kwenye mafunzo ya vyama vya msingi vya ushirika vya mikoa ya Lindi na Mtwara katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi, yanapofanyika maonesho ya 24 ya wakulima (Nane nane) kitaifa.
Ikiwa ni siku ya kwanza ya mafunzo hayo yanayotarajiwa kufanyika kwa siku tatu. Malunde alisema vya msingi vya ushirika (AMCOS) vinawajibu mkubwa wa kutoa elimu kwa wanachama wake, hasa viongozi na watendaji ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji na uongozi. Huku akibainisha kwamba kufanya hivyo sio hisani bali sheria inawataka wafanye hivyo kupitia fedha zake.
Alisema kwa kuzingatia ukweli huo utakaosababisha vyama kuwa imara na kuwa na uwezo wa kuwahudumia wanachana wake kwa ufanisi havina budi kutenga fedha kwenye bajeti zake ili zitumike kwa kazi hiyo muhimu.
Kaimu mrajisi huyo alibainisha kwamba kutokuwa na elimu kwa watendaji na viongozi wa AMCOS kunasababisha utendaji na uongozi mbovu katika baadhi ya vyama, na kusababisha migogoro, hasara na wanachama wake kujiondoa kutoka kwenye vyama hivyo.
“Msiwe mnategemea kuandaliwa na kuitwa kwenye mafunzo. Bali andaeni wenyewe ili muwajengee uwezo wa kiutendaji na uongozi viongozi na watendaji wenu. Kwamujibu wa sheria ya ushirika kunasehemu imeeleza bayana kuwa vyama vitumie sehemu ya mapato yake kwa ajili ya kutoa elimu ,” alisisitiza Malunde.
Mbali na hayo, Malunde alivikumbusha vyama hivyo kujenga mahusiano kwa jamii. Ikiwamo kutoa mrejesho kwa kuchangia shuguli za kijamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Huku Kaimu mrajisi huyo akiendelea kuwakumbusha kwamba vyama vya ushirika ni mali ya Wanachama. Kwahiyo ni vyombo huru vinatakiwa kufanya kazi bila kuingiliwa. Ambapo wenye haki, uwezo na mamlaka ya kufanya maamuzi ni wanachama wenyewe.
Maonesho ya Nanenane kitaifa katika viwanja vya Ngongo yameingia katika siku ya Tatu leo, baada ya kuzinduliwa juzi na waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene.

Post a Comment

 
Top