0
Rais Hassan RouhaniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Hassan Rouhani
Rais wa Iran Hassan Rouhani ameionya Marekani dhidi ya kuhatarisha mpango wa kinyuklia na viongozi wa mataifa yenye uwezo mkubwa duniani na kusema kuwa ni ''mshirika asiyeaminika'' .
Rouhani amemuambia rais Trump kwamba hatua zozote za kukandamiza mpango huo itamuangamiza kisiasa.
Amesema kuwa Iran itaendelea kuheshimu makubaliano ya mpango huo iwapo waliokubali kutia sahihi makubaliano hayo wataendelea kufanya hivyo.
Ikulu ya Whitehouse inasema kuwa Iran inaheshimu makubaliano hayo lakini rais Trump anasema kuwa taifa hilo linakiuka mpango huo.
Mwezi uliopita Marekani ilitangaza vikwazo vipya dhidi ya mpango wa Iran wa kinyuklia na kudai kwamba inaunga mkono makundi ya kigaidi.
''Hatua ya Marekani ya kutoheshimu utekelezwaji wa mpango wa kinyuklia...ni ishara tosha kwamba ni mshirika asiyeaminika kwa ulkimwengu na hata washirika wake wa siku nyingi'', alisema Rouhani katika sherehe ilioonyeshwa moja kwa moja na runinga ya taifa.
Rais huyo wa Iran aliyekuwa akiapishwa kwa mara ya pili baada ya kushinda uchaguzi mnamo mwezi Mei alisema kuwa hana haja ya kushindana na viongozi ambao hawajakomaa kisiasa na kuwataka viongozi waliokuwepo kuuona mpango huo kama mfano wa kusimamia uhusiano wa kimataifa.

Post a Comment

 
Top