0
Picha inayohusiana
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeshinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu ujao, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa ni wa mwisho wa kikosi hicho kabla ya kuelekea nchini Uganda kuweka kambi ya siku 10 katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya kuanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL),

Bao pekee la Azam FC limefungwa na beki kisiki na Nahodha Msaidizi, Aggrey Morris, dakika ya 57 kwa njia ya mkwaju wa penalti kufuatia mshambuliaji Wazir Junior kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Azam FC iliutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa hasa kipindi cha pili ikicheza soka safi la pasi na kasi huku ikishuhudiwa Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Junior, Enock Atta, Yahya Zayd, Bruce Kangwa, waking’ara vilivyo kwa kupeleka mashambulizi makali langoni mwa KMC.

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kinatarajia kupumzika kwa siku moja kabla ya keshokutwa alfajiri kuanza safari ya kuelekea nchini Uganda itakapocheza mechi nne za kirafiki dhidi ya KCCA, Vipers, URA na SC Villa, zote zikiwa timu kongwe za nchini humo.

Post a Comment

 
Top