0
Tanzania JULAI 5 imechapwa 4-2 na Zambia katika Mechi ya Nusu Fainali ya COSAFA CUP iliyochezwa huko Moruleng Stadium Nchini South Africa.
Licha ya kutangulia 1-0 kwa Bao la Erasto Nyoni la Dakika ya 14, Tanzania ilijikuta ikipigwa Bao za chapchap za Dakika za 44 na 45 kupitia Mwila na Shonga na kujikuta wako 2-1 hadi Haftaimu.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 56, Chirwa aliipa Zambia Bao la 3 kwa Penati na Shonga kufunga Bao la 4 Dakika ya 68.
Bao la Pili kwa Tanzania lilifungwa Dakika ya 84 na Simon Msuva.
Sasa Zambia wametinga Fainali na watacheza na Mshindi kati ya Lesotho na Zimbabwe wanaokutana baadae Leo.
Tanzania itagombea Ushindi wa 3 kwa kucheza na atakaefungwa kati ya Lesotho na Zimbabwe.
FAHAMU:
Hii ni mara ya 3 kwa Tanzania kucheza Mashindano haya baada ya kushiriki yale ya 1997 na 2015.
Nchi Wanachama wa COSAFA, South Africa, Swaziland, Botswana na Zambia waa Wenyeji South Africataanzia Hatua ya Robo Fainali ambapo South Africa itacheza na Mshindi wa Kundi A na Swaziland kucheza na Mshindi wa Kundi B wakati Botswana ikivaana na Zambia.
Mashindano ya COSAFA yalianzishwa Mwaka 1997 na Nchi za South Africa, Zambia na Zimbabwe kubeba Kombe mara 4 kila moja wakati Angola ikibeba mara 3 na Namibia mara 1.

Post a Comment

 
Top