Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika ikulu ya White House Sean Spicer amejizulu.
Taarifa zinasema amejiuzulu kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika kitengo hicho.
Bw Spicer ameng'atuka kutoka kwenye wadhifa wake kwa sababu hajaridhishwa na hatua ya Rais Donald Trump ya kumteua mkurugenzi mpya wa mawasiliano, kwa mujibu wa gazeti la New York Times.
Mshiriki mkuu katika soko la Wall Street Anthony Scaramucci ameteuliwa kuhudumu katika wadhifa huo ambao Bw Spicer alikuwa amefanikiwa kutekeleza tu sehemu ya majukumu yake.
Vikao vya Spicer na wanahabari vilikuwa maarufu sana kwa vyombo vya habari lakini hajahutubia wanahabari wiki za karibuni.
Mabadiliko kwenye kitengo hicho yametokea wakati ambapo ikulu ya White House inakabiliwa na tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa urais wa mwaka jana kumsaidia Trump kushinda.
Aidha, kuna tuhuma kwamba maafisa wa kampeni wa Trump huenda walishirikiana na maafisa wa Moscow.
Gazeti la New York Times linasema kuwa Spicer, 45, alipinga vikali kuteuliwa kwa Scaramucci.
Post a Comment