Na Asha Shaban,Musoma.
Mtoto wa miaka mitatu amefariki dunia kwa kupigwa na mama yake mzazi kwa tuhuma ya kula mboga mkoani Mara katika mtaa wa Songa mbele kata ya Rwamlimi katika Manispaa ya Musoma.
Tukio hilo lilitokea june 29 mwaka huu nyumbani kwa marehemu katika kata ya Rwamilimi majira ya saa mbili za usiku.
Hellena Magwita ni mama mzazi wa mtoto huyo inadaiwa mama huyo alimwadhibu mtoto wake kwa kosa la kula mboga aina ya furu,baada ya kipigo hicho mtoto alilia hadi akapoteza fahamu na mwishowe kupoteza maisha.
Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Songambele Bwana Frasinsico Owoko amekiri kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake huo nanakusema mtoto huyo alifariki dunia kutokana na kupigwa na mama yake kwa kosa la kula mboga nakupelekea kupoteza maisha.
Mwenyekiti alisema kuwa ni vyema wazazi wakawa makini huku akiaasa jamii kutoa taarifa mapema wanapokuwa wanaona matukio kama haya huku akisema kuwa asili ya mkoa wa Mara wamekuwa wakitumia hasira zao kutenda matukio kama hayo nakushindwa kujizuia.
"Wanatakiwa kutambua kuwa mkoa wetu wa mara nikati ya mkoa ambao umekuwa na watu ambao wanahasira lakini wanashindwa kujuzia hivyo kupelekea matatizo kujitokeza katika jamii zetu." alisema Owoko
Aidha mmoja wa wanandugu hao ambae hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa hakubaliani nakifo cha mtoto huyo eti kafariki kwa mchango kwani ukweli unafichwa ndani yake hivyo wataendelea kuchunguza ilikufahamu ukweli wa kifo cha mtoto huyo.
Kamanda wa polisi mkoani Mara Jafari Mohamed alisema mtuhumiwa huyo ameshiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na baada ya uchunguzi kukamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.
Post a Comment