0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Gao Mengdong akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ kwa mwaka 2017 inayoratibiwa na Kampuni hiyo kila mwaka leo jijini Dodoma. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei kwa mwaka 2017 jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Mkurugenzi wa kitengo cha TEHAMA wa chuo Kikuu Dodoma Dkt. Hector Mongi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (kulia) na Mkurugenzi wa Huawei Tanzania, Gao Mengdong wakitia saini kwenye mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika programu ya ‘Seeds for the future’ wakati wa hafla yauzinduzi wa programu hiyo iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo.Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (kulia) na Mkurugenzi wa Huawei Tanzania, Gao Mengdong wakipeana mkono baada ya kutia saini kwenye mkataba wa makubaliano wa kushirikiana wakati wa uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
Picha ya pamoja



Dodoma, 25 Julai, 2017:  Katika kuchangia maendeleo ya elimu nchini Tanzania, Kampuni ya Huawei inayoongoza ulimwenguni katika utoaji wa huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) leo imeendeleza juhudi zake kwa kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania kwa kuzindua programu yake ya kila mwaka ya ‘Seeds for the future’.

Uzinduzi wa programu hiyo umefanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Huawei imeeleza dhamira yake ya dhati katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Mafunzo ya Ufundi katika kupanua maarifa ya masomo ya TEHAMA kwa wanafunzi na watendaji wanaofanya kazi kwenye sekta ya Mawasiliano na Teknolojia.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, alipongeza juhudi za Huawei katika kuibua vipaji kwenye sekta ya TEHAMA nchini Tanzania na kushirikiana kikamilifu na wananchi.

Dkt. Akwilapo alimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ambao walitarajiwa kuzindua programu hiyo ya TEHAMA.

Dkt. Akwalipo alisema Huawei imekuwa mshirika muhimu waTanzania katika kukuza maendeleo ya TEHAMA nchini na imeendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika uvumbuzi wa masuala hayo kutokana na Serikali kuendelea kuboresha Teknolojia kupitia miradi yake mbalimbali.

“Ninapenda kuwashukuru Huawei kwa kile walichokianzisha na kuendeleza Programu ya ‘Seeds for the Future’ kwa wanafunzi wa Tanzania. Ninawahakikisha kwamba Wizara ya Elimu itaendelea kushirikiana na Huawei kwa sababu tunatambua kwamba TEHAMA ni muhimu sana pia katika kusaidia maendeleo ya elimu,”

Aliongeza kuwa Programu ya Seeds for the Future inaendeshwa na Huawei ulimwenguni kote kupitia kitengo chake cha Corporate Social Responsibility (CSR). Kupitia programu hii Huawei Tanzania imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wanafunzi 100 kutoka hapa nchini wanashiriki katika mradi wa miaka 10 ambapo inamaanisha kwamba kila mwaka wanafunzi 10 kutoka hapa nchini watapata fursa ya kutembelea Beijing na kufanya kazi na kampuni hii katika makao makuu yake yaliyopo Shenzhen, China.

Katika tukio hilo, Huawei pia ilisaini mkataba na Wizara ya Elimu kuhusu utekelezaji wa kukuza vipaji katika kuendeleza ICT unaojulikana ‘Huawei ICT Talent Cultivation Plan’ ambapo utawanufaisha vijana wenye taaluma, maofisa wa serikali na wahadhiri.

Malengo ya mpango huo ni kutekeleza programu ya kuhamasisha elimu ya TEHAMA iliyolenga kuinua kiwango cha elimu na kuendeleza mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma ICT. Hususani kukuza ushirikiano na Huawei ambao utaendeleza vituo vya mafunzo na kuanzisha madarasa maalumu katika ofisi za Huawei Tanzania.

Kupitia mkataba huo wa makubaliano uliosainiwa leo, tutaimarisha vituo vya kitaaluma katika ofisi za Huawei, Huawei Tanzania Customer Solution Intergration & Innovation Experience Centre (CSIC) na madarasa.

Zaidi ya hayo tutatoa nafasi za mafunzo kwa wanafunzi wa ICT kufanya kazi za muda katika ofisi za Huawei Tanzania jambo ambalo litawasaidia kujifunza, kufanya tafiti na kuendelea ujuzi wao kwenye masuala ya TEHAMA,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Bwana Gao Mengdong.

Aidha, Huawei pia imedhamiria kutimiza ahadi yake ya kupanua ushirikiano wake na serikali katika kuanzisha mradi wa mafunzo kwa matandao ambao ushirikiano huo utatoa mchango mkubwa zaidi kwa sekta ya elimu nchini Tanzania na maendeleo ya ICT ili kuifanya Tanzania kufikia malengo ya dira ya maendeleo ya mwaka 2025.

Kwa mujibu wa Gao, falsafa ya Huawei ni ‘Expoloration’ ikiwa na maana kwamba kampuni itaendelea kubuni kila namna ili kuiwezesha nchi kuendelea kutimiza mipango yake ya maendeleo.

Miongoni mwa wanafunzi walioteuliwa kushiriki programu hii, Kadhija Mohammed aliipongeza Huawei kwa kuendelea kuibua vipaji vya ICT nchini Tanzania na kuendelea kushirikiana na wananchi.

Alisema Huawei imekuwa msharika muhimu kwa maendeleo ya ICT nchini Tanzania na imeendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika uvumbuzi wa ICT ambapo serikali imekuwa ikiendelea kuboresha ICT kupitia miradi yake mbalimbali.
“Ni matumaini yetu kwamba Serikali ya Tanzania itatumia vyema fursa iliyotolewa na Huawei na tunaamini kupitia Programu ya Seeds for the Future tutajifunza mambo mengi kutoka kwa Huawei Tanzania,” alisema.

Post a Comment

 
Top