Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 26 ya Biko, Leonard Bagumako wa pili kutoka kulia. Wengine pichani ni baba mlezi wa Bagumako, Gerlad Madaraka kushoto pamoja na mtumishi wa NMB, Tawi la Bank House, jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 20 kutoka Bahati Nasibu ya Biko, Leonard Bagumako, amesema ameyavulia kofia mamilioni ya Biko, baada ya kukabidhiwa huku akiwa hakufahamu lolote kwamba yeye angeweza kuyatwaa.
Bagumako aliyasema hayo jana wakati anakabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 20, katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam, huku akiwa kijana mwenye umri wa miaka 21 tu anayefanya shughuli za uuzaji wa duka Kigamboni.
Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 26 ya Biko, Leonard Bagumako katikati. Kushoto ni baba mlezi wa Bagumako, Gerlad Madaraka. Picha na Mpigapicha wetu.
Akizungumzia fedha hizo, Bagumako alisema awali aliamini kuwa mchezo wa Biko unahusu watu matajiri, lakini baada ya kukabidhiwa fedha hizo, ameamini kila Mtanzania bila kuangalia wapi anaishi na uchumi wake anaweza kuibuka kidedea kwa kupata ushindi.
“Biko nimewavulia kofia kwa sababu kumbe hata sisi mafukara tunaweza kushinda zawadi mbalimbali za biko kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja za papo kwa hapo, bila kusahau ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kama niliyoupata mimi,” Alisema.
Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema baada ya kumkabidhi Bagumako fedha zake, wanashauku kubwa ya kumkabidhi mtu mwingine Milioni 20 atakayetokana na droo ya 27 itakayofanyika Jumapili, jijini Dar es Salaam.
“Bagumako ameshapata fedha zake na mwingine atapokea kutoka droo kubwa ya Jumapili, ambapo Biko tunaamini yoyote anaweza kuibuka na ushindi huo mnono kwa kucheza biko kwa mitandao ya simu Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.
“Namna ya kucheza ni rahisi kwa sababu mshiriki atafanya muamala kulingana na matakwa ya mtandao wake, huku kiasi cha Sh 1,000 kikiwa na nafasi mbili, ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 inayofanyika Jumapili na Jumatano,” Alisema.
Kwa kipindi cha miezi miwili ya Mei na Juni, tayari bahati nasibu ya Biko, wameshatoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wa papo kwa hapo na donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili.
Post a Comment