0
MorataHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAlvaro Morata alifungia Real Madrid mabao 20 msimu uliopita
Chelsea wamefikia makubaliano kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata kwa ada inayoripotiwa kuwa £70m.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uhispania sasa anatakiwa kuafikiana masuala yake ya kibinafsi na klabu hiyo na pia achunguzwe hali yake ya kiafya kabla ya kukamilisha uhamisho wake.
Morata, 24, atakuwa mchezaji wa nne kununuliwa na mabingwa hao wa Ligi ya Premia majira haya ya joto, baada ya kipa Willy Caballero, beki Antonio Rudiger na kiungo wa kati Tiemoue Bakayoko.
Morata alifunga mabao 20 msimu uliopita baada ya kujiunga na Real kutoka Juventus.
Alishinda taji la La Liga na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita, lakini mara nyingi alikuwa akicheza kama nguvu mpya.
Morata huenda akachukua nafasi ya mwenzake wa Uhispania Diego Costa, ambaye anasema aliambiwa na meneja wa Chelsea Antonio Conte kwamba hayupo tena katika mipango ya klabu hiyo.
Manchester United walikuwa wakitaka kumnunua Morata kabla ya kumnunua mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku kwa £75m.
Morata alijiunga na timu ya wachezaji chipukizi Real Madrid mwaka 2008 na akachezeshwa timu kubwa akiwa na miaka 18 mwaka 2010.
Mshambuliaji huyo mwenye kimo cha futi 6 na inchi 3 alihamia Italia mwaka 2014 na kufunga mabao 27 katika miaka miwili aliyokaa Juventus.
Kipindi hicho alishinda Serie A na Coppa Italia mara mbili na pia alicheza katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2015.
Real walitumia kifungu cha kumnunua tena kumnunua Juni 2016 na kumrejesha Bernabeu.
Morata amechezea taifa lake mechi 20 na kfuunga mabao tisa tangu alipoanza kuwachezea mwaka 2014.

Wachezaji walionunuliwa ghali zaidi duniani

£89m - Paul Pogba - Juventus kwenda Manchester United, 2016
£86m - Gareth Bale - Tottenham kwenda Real Madrid, 2013
£80m - Cristiano Ronaldo - Manchester United kwenda Real Madrid, 2009
£75.3m - Gonzalo Higuain - Napoli kwenda Juventus, 2016
£75m - Luis Suarez - Liverpool kwenda Barcelona, 2014; Romelu Lukaku - Everton kwenda Manchester United, 2017

Post a Comment

 
Top