0
Diego CostaHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, atakaidi hatua ya Antonio Conte na kukataa kuondoka Stamford Bridge, hadi akubaliwe kurudi Atletico Madrid (Daily Star).
Diego Costa amewaambia Atletico Madrid kuwa anataka kurejea Spain. Kutokana na Atletico kufungiwa kusajili, hata akisajiliwa sasa hatoweza kucheza hadi Januari (Sky Sports).
Thibault Courtois hajasaini mkataba mpya, huku Real Madrid wakimnyatia. Kipa huyo wa Chelsea anataka mkataba wa pauni milioni 10 kwa mwaka (The Sun).
Real Madrid wanasubiri Manchester United kupanda dau la kumtaka mshambuliaji Alvaro Morata, 24, kabla ya mabingwa hao wa Ulaya kuanza kumfuatilia Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Diario Gol).
MbappeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKylian Mbappe (kushoto)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane atafikiria kuimarisha safu ya ulinzi kwa kumchukua Leonardo Bonucci kutoka Juventus. Zidane hana mpango wa kusajili mabeki wengine na atatoa nafasi kwa chipukizi ikiwa hawatoafikiana na Juve (Diario Gol).
Hatua ya Ronaldo kubadili mawazo ya kuondoka Real Madrid, imelazimisha Manchester United sasa kuzingatia zaidi usajili wa Alvaro Morata. Jose Mourinho tayari ametenga pauni milioni 60 na wanadhani watamchukua kabla ya mechi za kabla ya kuanza kwa msimu (The Sun).
Cristiano Ronaldo anafikiria kwenda Paris Saint Germain baada ya kupewa dau na klabu hiyo (Marca).
Alvaro MorataHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlvaro Morata alitarajiwa kuhamia Manchester United
Jose Mourinho ameiambia Manchester United kuachana na Ronaldo na kulenga kumsajili Neymar badala yake (Don Balon).
Juventus wamepiga hatua za mwanzo katika jitihada zao za kutaka kumsajili Matteo Darmian kutoka Manchester United (Sky Sport Italy).
Kiungo wa Manchester City Samir Nasri anatarajiwa kupewa mshahara wa pauni 275,000 kwa wiki, baada ya kukatwa kodi, ili kujiunga na Shanghai Shenhua ya China (The Sun).
Manchester United wamekuwa na mazungumzo na wakala wa Robert Lewadowski katika jitihada za kutaka kumchukua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland na Bayern Munich (Sky Sports).
Zlatan Ibrahimovic anataka kwenda Real Madrid baada ya kuruhusiwa kuondoka Manchester United (Diario Gol).
Samir NasriHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSamir Nasri
Mustakbali wa Robert Lewandowski kusalia Bayern Munich utategemea na matokeo ya klabu hiyo ya Ujerumani kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez (The Sun).
Leicester City wanapanga kutoa pauni milioni 25 kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20 (Daily Telegraph).
Leicester wanafikiria hatua ya kuchukua baada ya West Brom kuwaambia watahitaji kutoa pauni milioni 10 ikiwa wanamtaka beki Jonny Evans, 29 (Leicester Mercury).
Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kutoka Monaco kwa pauni milioni 35, hatua ambayo huenda ikasababisha Nemanja Matic, 28, kuondoka na kwenda Manchester United (Daily Mail).
Sakata la Manchester City kumtaka beki wa Tottenham Kyle walker, 27, litaendelea hadi wiki ijayo baada ya Spurs kukataa kushusha bei ya pauni milioni 50. Hata hivyo City wataendelea kumfuatilia pia Dani Alves kutoka Juventus (Independent).
Manchester City wapo tayari kupokea pauni milioni 18 kutoka Lyon ili kumuuza Eliaquim Mangala. City walimnunua Mangala kwa pauni milioni 42 miaka mitatu iliyopita (SportsMole)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Post a Comment

 
Top