Klabu ya Swansea City imekubali kumasajili mshambuliaji Tammy Abraham kwa mkopo kutoka Chelsea kwa msimu wa 2017-2018.
Swansea wamekabili upinzani kutoka kwa Newcastle na Brighton kwa mshambuliaji huyo wa miaka 19 ambaye alifunga mabao 23 katika mechi 40 akiwa kwenye mkopo na klabu ya Bristol City msimu wa 2016-2017.
Mpango huo unatarajiwa kukamilika leo.
Abraham alifanya kazi na Paul Clement wakati meneja huyo wa Swansea alikuwa kocha huko Stamford Bridge.
Post a Comment