Madai ya ufisadi
katika mafanikio ya Qatar kuandaa kombe la dunia la 2022 yamechapishwa
katika vyombo vya habari nchini Ujerumani.
Gazeti la The Bild
linasema kuwa ripoti hiyo ya 2014 ''iliokandamizwa'' iliandaliwa na
aliyekuwa afisa huru wa maadili katika shirikisho la soka duniani
Michael Garcia.
Ripoti hiyo ya Bild inashirikisha maelezo ya kitita cha $2m kilicholipwa mtoto wa miaka 10 wa afisa mmoja wa Fifa.
Garcia alijiuzulu mwezi Disemba 2014 akipinga vile ripoti yake ilivyochukuliwa kuhusu zabuni za kuandaa michezo hiyo.
Wakili
huyo wa Marekani alishutumu ukosefu wa uongozi bora katika shirikisho
hilo wakati alipoondoka, huku viongozi hao wakichapisha ripoti nyengine
kama hiyo ambayo iliiondolea makosa yoyote ya ufisadi Qatar.
Gazeti hilo la Bild limesema kuwa litakuwa likichapisha maelezo ya ripoti hiyo ya Garcia yenye kurasa 403 kuanzia Jumanne ijayo.
Post a Comment