Aliyekuwa waziri
mkuu nchini Tanzania na mwanachama wa Chama cha Chadema Edward Lowassa
amewasili katika afisi ya mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai baada ya
kutakiwa kufika katika afisi hiyo siku ya Jumatatu kwa sababu
zisizojulikana .
Kulingana na gazeti la The Citizen, Bwana Lowassa
ambaye alitakiwa kuwasili katika afisi ya DCIO muda wa saa nne
aliwasili saa tatu na dakika 58 asubuhi.
Msafara wake ulikuwa na magari sita ikiwemo magari mawaili ya polisi yaliokuwa na na polisi waliojihami .
The Citizen linasema kuwa usalama ulikuwa umeimarishwa katika barabara ya Ohio.
Waandishi habari walikatazwa kuchukua picha za bwana Lowassa.
Katika
mahojiano ya simu na gazeti la The Citizen, alisema kuwa anashuku
kwamba agizo hilo la kutakiwa kujiwasilisha linatokana na matamshi
aliyotoa mjini Dar es salaam siku ya Ijumaa wakati wa hotuba ya Iftar.
Wakati
wa hotuba hiyo, alimtaka rais Magufuli kuwaachilia huru wahubiri wa
Kiislamu ambao walikuwa wamekamatwa kwa zaidi ya miaka minne bila kesi
zao kuamuliwa.
Post a Comment