China imeishutumu
India kwa kuvamia himaya yake kati ya Sikkim na Tibet katika mzozo ambao
umezua hali ya wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.
Maafisa
wanasema kuwa walinzi wa mipakani waliingilia hali ya kawaida katika
himaya ya China na kuitaka India kuondoka mara moja.
India hivi karibuni iliwashutumu wanajeshi wa China kwa kuingilia eneo lake.
Eneo hilo ,kwa jina Nathu La Pass hutumiwa na mahujaji wa India wanaoelekea katika maeneo ya Hindu na Budha huko Tibet.
Eneo hilo lilikumbwa na mgogoro kati ya China na India 1967 na wasiwasi uwepo mara kwa mara.
Muhariri
wa Kusini mwa Asia Ethirajan Anbarasan anasema kuwa kisa cha hivi
karibuni kinaonekana kuwa mgogoro mbaya zaidi kati ya mataifa hayo
mawili katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.
Reuters imenukuu maafisa wa China waliosema kuwa kisa hicho huenda kikatishia kuwepo kwa amani.
China imeshutumu India kwa kuzuia ujenzi wa barabara katika eneo inalosema liko upande wake mpakanni mwa nchi hizo.
Hakujakuwa na tamko rasmi kutoka kwa India kuhusu madai hayo kufikia sasa.
Kulingana
na vyombo vya habari nchini India ,kumekuwa na hali ya wasiwasi kati ya
walinzi wa mpakani kutoka pande zote mbili katika wiki za hivi karibuni
huku vikosi vya China vikidaiwa kuvuka na kuingia katika eneo la Sikkim
na kuharibu mahandaki ya jeshi la India.
Wasiwasi uliopo umeilazimu Beijing kuzuia mahujaji kuelekea katika eneo hilo la mpakani.
Post a Comment