Mshike mshike wa michuano ya kombe la mabara umeingia siku ya pili huko nchini Urusi, ambapo leo kumechezwa michezo miwili ya mashindano hayo yanayoshirikisha timu nane.
Katika kundi A timu ya taifa ya Ureno walitoshana nguvu na Mexico kwa sare ya mabao 2-2, Ricardo Quaresma alianza kuipatia Ureno goli la kuongoza katika dakika ya 35
Mexico walisawazisha goli hilo kupita kwa Javier Hernandez Chicharito na kumfanya mshambuliaji huyu kuwa ndio mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa akifikisha mabao 48.
Beki Cedric Soares akaongeza bao la pili kwa Ureno katika dakika ya 86 kabla ya Hector Moreno kusawazisha goli hilo kwa upande wa Mexico katika dakika za lala salama.
Katika mchezo wa kundi B wawakilishi wa bara la Afrika Cameroon walichapwa na mabingwa wa Amerika ya kusini, Chile kwa mabao 2-0 mabao ya Chile yalifungwa katika kipindi cha pili na Arturo Vidal na Eduardo Vargas.
Post a Comment