- Real Madrid sasa imo njiani kuwa timu ya kwanza katika bara la Ulaya kutetea taji lao la Champions League baada ya kukata tikiti yao katika fainali dhidi ya Juventus Turin mjini Cardiff
Ni mara ya tatu kwa Real Madrid kuingia katika fainali katika muda wa miaka minne, ambayo imefikia licha ya ushindi wa mahasimu wao Atletico Madrid wa mabao 2-1 jana Jumatano.
Real Madrid imevuka kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2. Real Madrid iliwashinda mahasimu wao hao kutoka mjini Madrid katika fainali ya mwaka jana na pia mwaka 2014, na pia iliwatoa katika awamu ya robo fainali mwaka 2015.
Katika nusu fainali ya kwanza, Juventus Turin iliishinda AS Monaco. Wataliani walionesha uwezo wao mkubwa katika mchezo huo ambao ulipigiwa upatu kuwa ni kati ya uwezo wa ulinzi dhidi ya uwezo wa ushambuliaji na kushinda kwa mabao 2-1.
Mabao ya Mario Mandzukic na Dani Alves yaliweza kuua uwezo wa Monaco katika kipindi cha kwanza. Juventus ina matumaini ya kushinda taji hilo katika muda wa miaka 21 mwezi ujao mjini Cardiff.
Post a Comment