
Baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake
zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi
nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado
fedha inakosa thamani.
Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa
kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa
kulinganisha na nchi nyingine duniani. April 1 2017 nakuletea list
ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa
kuliko nchi nyingine.
7: Rand – Afrika Kusini (1$=14)
Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una
nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa
kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake
kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja
kwa Rand 14.

6: Pula – Botswana (1$ = 10.8)
Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana
ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokanayo na uchimbaji wa
madini na ufugaji. Dola moja huuzwa kwa Pula 10.8.

5: Dihram – Morocco (1$=9.9)
Morocco ni moja kati ya nchi ambazo zinajivunia kuwa na
fedha yenye thamani barani Afrika ambapo uchumi wake unatokana na
kujijenga kwa sekta za Utalii, Viwanda na Kilimo. Dola moja ni sawa na
Dihram 9.9.

4: Kwacha – Zambia (1$ = 9.84)
Kwacha ni moja kati ya sarafu maarufu sana Kusini mwa
Afrika ambayo hutumika nchini Zambia. Sarafu ya Kwacha imekuwa na nguvu
sana na thamani kutokana na uchumi mkubwa wa nchi hiyo unaotokana na
mapato katika sekta ya Utalii. Dola moja ina thamani ya Kwacha 9.84.

3: Pound – Sudan (1$=6.4)
Licha ya kuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa muda
mrefu lakini Sudan imendelea kuifanya sarafu yake kuwa na thamani na
yenye nguvu zaidi katika kipindi cha miaka mingi kutokana na uchimbaji
wa mafuta ambayo yanauzwa nje ya nchi, Uvuvi, na Kilimo ambavyo ni
vyanzo vya mapato ya nchi. Dola moja hununuliwa kwa Pound 6.4 za Sudan.

2: Cedic – Ghana (1$= 4)
Ghana ndiyo nchi pekee ambayo imeingia kwenye list ya nchi
zenye sarafu yenye thamani na nguvu kubwa Afrika kwa upande wa nchi za
Afrika Magharibi ikikamata nafasi ya pili. Hivi karibuni nchi hiyo
imegundua mafuta hivyo kuwaongezea mapato zaidi bila kujali kama bidhaa
zao zimeshuka kwenye mauzo. Nchi hiyo inajivunia kuwa na Demokrasia
imara barani Afrika hivyo imejiimrisha vizuri katika uchumi. Dola moja
hununuliwa kwa Cedic 4.

1: Dinar – Libya (1$= 1.4116)
Dinar ambayo ni fedha ya Libya inakamata nafasi ya kwanza
kwa kuwa fedha yenye thamani na nguvu kubwa barani Afrika ambapo Dola
moja hubadilishwa kwa Dinar 1.4116.

Post a Comment