0
 Ligi la mchezo wa mpira wa miguu Three Boys Cup 2017 leo mei 28 limeanza kutimua vumbi kwa kuwakutanisha timu ya Mitumba fc dhidi ya Red star,mchezo uliopigwa uwanja wa halmshauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika mchezo huo timu ya red star ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu goli lililofungwa na Mawazo Kiwima na magoli ya timu ya Mitumba fc yakifungwa na Masudi Mbwana,Saidi Milasi na goli la tatu likifungwa na Huseni Mchite.
 Mchezaji wa timu ya Red star akijaribu kutoa pasi ili kuweza kusawazisha goli lakini jitihada ziligonga ukuta baada ya timu ya Mitumba fc kuimalisha ukuta wao
 Mchezaji wa timu ya Mitumba fc akimiliki mpira


 Mchezaji wa timu ya Mitumba fc,Hamza Lipupu akiwa chini baaada ya kuchezewa rafu






Waamuzi wa mchezo wakipongezana baada ya kumalizika kwa mchezo huo

Post a Comment

 
Top