0

Wanachama wa chama cha ushirika cha msingi Umoja zaidi ya 770 walioudhulia mkutano mkuu wa chama uliofanyika katika ghala mkuu la chama hicho jana mei 15 mwaka 2017


Wanachama wa chama cha ushirika cha msingi Umoja zaidi ya 770 walioudhulia mkutano mkuu wa chama uliofanyika katika ghala mkuu la chama hicho jana mei 15 mwaka 2017
  Katibu tawala wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Mbwana Kambangwa akisaini kitabu cha wageni 

       Afisa ushirika wilaya ya Liwale,Mohamedi  Nanjinji
Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha msingi umoja Bwana Hassani Mpako aliyetetea kiti chake na kuweza kupata ridhaa ya wanachama wa chama hiko kuendelea na kuwasimamia.

Wanachama wa chama cha ushirika cha msingi Umoja ­(Umoja Amcos­­) wametakiwa kuendeleza ushirikiano na mshikamano na viongozi wao katika kufanya maendeleo kwa vitendo.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama cha umoja jana mei 15 katibu tawala wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Bwana Mbwana Kambangwa alipokuwa anatoa nasaa za serikali kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Mheshimiwa Sarah Chiwamba.

“Wanachama pamoja na viongozi mushirikiane  kwa sababu hatua muliyoifikia hakuna chama cha msingi kilichofikia toka uhuru katika kuchangia masuala ya maendeleo kwa vitendo katika jamii ”Alisema Kambangwa.

Kambangwa aliwasii wanachama wa chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu kufanya maaamuzi sahihi katika kuwapata viongozi wanaofaa watakao weza kusimamia miradi mbalimbali ya chama hicho kwa maslahi ya wanachama wote.

Wanachama wa umoja waliweza kufanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa ngazi mbalimbali,afisa ushirika wilaya ya Liwale, ndugu Mohamedi Nanjinji alisimamia uchaguzi huo kwa uhuru,haki na amani kuanzia ngazi ya wajumbe wa bodi,mwenyekiti pamoja na makamo mwenyeki.

Baada ya kufanya uchaguzi wanachama wa umoja waliendelea kuwaamini wajumbe wa awali huku nafasi ya mwenyekiti iligombewa na Bwana Hassani Mpako  na makamo mwenyekiti ikigombewa na Bwana Saidi Timutimu walipigiwa kura za ndio au hapana na kupita bila kupingwa.

Mwenyekiti aliyetetea kiti chake Bwana Hassani Mpako mara baada kuchaguliwa tena aliangusha machozi akisema wamempa dhamana ya kuendeleza chama hicho akiongeza kusema amebeba mzigo mkubwa sana katika kusimamia haki na kulinda maslahi ya wakulima.

Mpako aliwaomba wajumbe wake wa bodi kufanya kazi kwa umoja,ushirikiano na umakini wa hali ya juu  na kurekebisha kasoro zote ndogondogo kutokana na dhamani ya wanachama waliowapa.

Baadhi ya wanachama wa cha umoja Zainabu Mandepe na Mohamedi Athumani wakizungumza kwa niaba ya wanachama wamesema wahasibu wa chama hicho wanatakiwa kupewa mafunzo zaidi ili kuweza kufanya kazi kwa uhakika na kuweza kukifanya chama chao kusonga mbele zaidi pia wakiomba wanachama kupewa semina mbalimbali ili kuweza kupata elimu na kuweza kuongeza uzalishaji.

Post a Comment

 
Top