0

Kituo cha radio NACHINGWEA FM 90.9 kinachomilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kimetakiwa kuzima mitambo yake mpaka pale mafundi watakapomaliza kufunga mitambo yote licha ya kituo hicho kufikia hatua nzuri na muhimu sana kwa dunia ya sasa katika upashanaji habari kwa kuweza kununua vifaa vya radio na television.

Hatua ya sasa vifaa hivyo vya radio vimewashwa lakini bila kumalizika kufungwa hali inayopelekea baadhi ya maeneo wilayani humo kuyanasa mawimbi hayo ya radio katika 90.9 Nachingwea FM.

Licha ya KUANZA kusika kwa baadhi ya maeneo lakini kunaibuka na maeneo yanayoonesha kama  kuna udhaifu uliojitokeza mpaka watu wakaanza  maneno kwa kulalamika kuwa kuna mchemko ni kutokana na transmission antenna ipo hewani chini ya futi 100 hivyo mawimbi yanakutana na viathiri vibeba mawimbi (propagation of carrier wave).

Kwa kuwa mafundi wapo kazini hawajamaliza kazi ya ufungaji mitambo hiyo wakazi hao wanahitaji huduma bora ya radio baadhi ya wadau wilayani humo ndugu Victor Richard ameshauri wakati mafundi wanaendelea kufunga mitambo hiyo wangezima mitambo hiyo hadi hapo utakaposimikwa mnara na antenna zote zikiwa zimetimia na kuzingatia usalama wa radio na usalama wa anga ndipo waanze  kufanya majaribio.
''Wakati mchakato wa mnara unafanyika uendane sambamba na upatikanaji wa nishati ya kudumu itakayosaidia wakati wote ambao hautakuwepo umeme huu wa kisiasa ili radio iweze kufanya kazi muda wote pia kuingia kwenye ushindani na radio mbalimbali hapa nchini mfano Clouds FM'' alisema Richard.

Pia alisisitiza suala la kuwepo ulinzi maalum kwa ajili ya kituo cha radio amesema  bila kutegemea walinzi wa ujenzi ikiendana na uzio madhubuti.

Pia ameshauri wakati kituo hiko kinatafuta watangazaji kisimsahau kutoa kipao mbele kwa watangazaji wazawa ambao watakao kuwa na sifa kwa kufuata  sifa ya elimu ya habari angu kwakuwa radio zinaelekea kwenye ulimwengu wa ushindani.

Post a Comment

 
Top