0
Tokeo la picha la Gareth Bale
Msimu ujao ni muhimu sana kwa Gareth Bale kuwa fit na kurejesha kiwango chake pale Real Madrid kwa mujibu wa mchambuzi wa soka la Hispania, Terry Gibson


Mshambuliaji huyo amekuwa akiandamwa na janga la majeraha la mara kwa mara na kusababisha kucheza mechi 26 tu katika mashindano yote msimu huu na akifunga magoli 9 tu.

Lakini msimu huu ukionekana sio kuwa mzuri kwa Bale , mchambuzi huyo wa Sky Sports , Gibson amesema kwamba Bale anatakiwa kufikiria zaidi msimu ujao na kuwa fiti zaidi ili kurejesha kiwango chake na kufunga midomo ya wanaotia shaka uwezo wake.

"Muda kama huu msimu uliopita tulikuwa tunajadili kama Bale yupo kwenye daraja sawa na Neymar , mmoja wa wachezaji ambao watakuja kuchukua mikoba ya Ronaldo na Messi kama wachezaji bora Duniani. Ameandamwa sana majeraha."

"Msimu ujao ni muhimu sana. hicho ndio kimemzuia kufunga magoli ukiangalia takwimu zake kwasababu hajacheza idadi nzuri ya mechi ambazo angependa kucheza kwa sababu ya majeraha."

"Msimu ujao ni mkubwa sana kwa Bale . Sio rahisi kumuambia mchezaji ' Unatakiwa kuwa fiti ' kwasababu kila mchezaji anataka kuwa fiti na wanafanya kila wawezalo lakini amekuwa na bahati mbaya sana na labda walimuharakisha mapema kwenye mechi ya Clasico na hiyo haikumsaidia kabisa."


"Nataka kumuona Bale akiwa fiti , nataka kumuona akiwika tena Real Madrid lakini hawezi kukubali tena msimu ujao acheze mechi 26 tu na magoli machache na kukosa muda mwingi wa kucheza kutokana na majeraha. Baada ya hapo nadhani maswali yataulizwa."

Post a Comment

 
Top