0
Trump kuongeza bajeti ya jeshi kwa dola bilioni 54Trump kuongeza bajeti ya jeshi kwa dola bilioni 54
Rais wa Marekani Donald Trump amaeahidi kile alichokitaja kuwa nyongeza ya kihistoria kwa bajeti ya jeshi la Marekani.
Maafisa wa ikulu ya White House wanasema kuwa bajeti ya ulinzi nchini Marekani itaongezeka kwa dola bilioni 54, ikiwa ni karibu asilimia 10.
Fedha hizo zitapatikana kwa kupunguza bajeti za programu zisizo za kijeshi, ikiwemo misaada ya kigeni na fedha zinazotumiwa kwa utunzi wa mazingira.
Mipango hiyo itawasilishwa kwa bunge la Congress mwezi ujao.
Wakati huo huo idara ya ulinzi imewasilisha kwa White House, mipango ya kulishinda kundi la Islamic State ambayo Rais Trump alikuwa ameitaka idara hiyo kuishughulikia.
Haki miliki ya picha Getty Images
 
Marekana inatumia fedha nyingi zaidi kwa ulinzi kuliko nchi yoyote
Marekana inatumia fedha nyingi zaidi kwa ulinzi kuliko nchi yoyote

Post a Comment

 
Top