Rais wa Marekani
Donald Trump amekubali kuheshimu kile anachokiita sera ya "China Moja"
pale alipompigia simu Rais wa China Xi Jinping, Ikulu ya White House
imesema.
Sera ya China Moja ni elimu ya kidiplomasia, kwamba kuna serikali moja tu iitwayo China.
Bwana Trump alitilia shaka sera ya muda mrefu ya china, pale alipofanya mazungumzo na Rais wa Taiwan ,mwezi Desemba.
Hiyo
ni mojawepo ya hatua kubwa mno ya kuvunja tamaduni ya muda mrefu ya
kufuata taratibu ya uongozi, na kuchochea malalamiko rasmi kutoka kwa
utawala wa China.
Mazungumzo hayo ya simu ni ya kwanza kati ya
marais hao wawili tangu Trump alipoingia ofisini Januari 20, licha ya
Rais Trump kuwapigia simu viongozi wa mataifa kadhaa duniani.
Ikulu ya White House inasema kuwa maswala mbalimbali
yalijadiliwa wakati wa mazungumzo hayo ya simu ambayo ilitajwa kama "
mzuri sana ".
Viongozi hao wawili walialikana kuzuru mataifa yao, inasema taarifa hiyo, huku wakitarajia kuendeleza zaidi mazungumzo yao.
Taarifa kutoka Beijing zinasema kwwamba, China inampongeza Bw Trump kwa kutambua sera ya China Moja.
Mataifa
haya mawili "washirika wa karibu, na kupitia juhudi za pamoja,
tunaweza kuboresha Zaidi uhusiano huu na kufikisha katika kiwango cha
juu zaidi katika historia", Taarifa hiyo ilimnukuu Bw Xi.
Mazungumzo
hayo ya simu yalifuatia barua iliyotumwa na Bw Trump kwa Rais Xi hapo
jana Ahlamisi- hatua ya kwanza ya Trump kumfikia kiongozi huyo wa China.
Awali Bw Trump alisababisha taharuki kubwa mno na
Beijing, wakati alipokubali mawasiliano ya simu kutoka kwa kiongozi wa
Taiwan Tsai Ing-wen.
Hata ingawa Marekani ni mshirika wa karibu wa kijeshi na Taiwan, hakuna Rais au Rais mteule wa Marekani amewahi kuzungumza moja kwa moja na kiongozi wa Taiwan, kwa miongo kadhaa.
Hata ingawa Marekani ni mshirika wa karibu wa kijeshi na Taiwan, hakuna Rais au Rais mteule wa Marekani amewahi kuzungumza moja kwa moja na kiongozi wa Taiwan, kwa miongo kadhaa.
Post a Comment