Somalia imesitisha
safari za ndege zinazoingia na kutoka katika Uwanja wa Ndege wa
Mogadishu, siku ya Jumatano ambapo uchaguzi wa Rais utafanyika.
Ikiwa ni wa kwanza kufanyika katika kipindi cha miaka 25.
Mahala
uchaguzi utakapofanyika ulihamishwa kutoka katika makao makuu ya polisi
hadi katika uwanja wa ndege kutokana na sababu za kiusalama.
Waziri
wa Usafiri Ali Jama Kangali ameiambia BBC kwamba hakuna ndege
zitakazoruhusiwa katika uwanja wa Mogadishu, siku hiyo ya Jumatano
wakati uchaguzi ukiendelea.
Kumekuwa na wasiwasi kwamba wapiganaji wa Al Shabaab wanaweza kufanya mashambulio kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo.
Wapiganaji
hao kwa sasa wamekuwa wakiwalenga na kuwaua wanasiasa, raia na
wanajeshi kwa kutumia risasi na milipuko. Wamekuwa wakiipinga serikali
ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Wabunge 329 wa Somalia watamchagua rais mpya wa nchi hiyo kati ya wagombea 24 wanaowania kiti hicho.
Hali ya kutokuwepo na usalama imesababisha kushindwa kwa watu wote nchini humo kupiga kura kumchagua rais.
Post a Comment