NA KENNETH NGELESI,RUNGWE
MWANAMKE
Vaileth Michael Kyotamawe (29) mkazi wa mtaa Tandale kata ya Kiwila
Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya,amemwagiwa maji ya moto na kuunguzwa
mgongoni na makalioni na wifi yake dada wa Mume wake Elizabeth Mwatebela
kwa kile kinacho elezwa ni kutokana na tatizo la kuto kuzaa.
Akizungumza
na eddy blog Baba mzazi wa Vaileth,Michael Kyola alisema kuwa tukio
hilo la kikatili limetokea Jenuari 23 mwaka huu majira ya saa 12:00
jioni na nyumbani kwa wazazi wa mume wa Vaileth katika Mtaa wa Tandale
Ibula Kata ya Kiwila Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Alisema
Chanzo cha ugomvi ni kutokana Vaileth kutumiwa ujumbe mfupi wa matusi
na Wifi yake Elizabeth ambaye ni dada wa Mumewe kwa njia ya simu ya
mkononi akimtukana na kumwambia hakuna sababu ya kuendelea kuishi na
kaka yao wakati hazai na kwamba anamfilisi.
Kyola
alisema Vaileth ambaye ameolewa na James Mwatebela kwa zaidi ya miaka
minne bila kujaliwa mtoto alienda kwa wakwe kwa ajili ya kueleza hali
hiyo,na alipofika nyumbani hapo aliwakuta mama mukwe na wifi huyo na
kuanza kumuuliza wifi yake kwanini anamtukana? na kuhoji yeye kuto zaa
watoto wakati mwenye haki hiyo ni kaka yake na siyo yeye.
Alisema wakati akihoji swali hilo alijibiwa na Elizabeth kuwa alikuwa anamtafuta siku nyingi hivyo alikuwa amejipeleka.
Aliongeza
baada ya hapo walianza kurushia maneno ya hapa na pale,lakini kwa kuwa
ugomvi huo ulikuwa na Baraka za mama Mukwe walisikiana na Eliabeth
aliyekuwa amebeba mtoto alimshusha na kumkabidhi mama yake na kumvaa
Vaileth na ndipo ugomvi ukaanza.
‘Vaileth
amekuwa akitumiwa ujumbe mfupi wa matusi mara kwa mara na wifi yake
huyo kwa njia ya simu ya mkononi kuhusiana na yeye kuto zaa na siku hiyo
baada ya uvumilivu kumshinda alifunga safari kwenda kwa wakwe kwa ajili
ya kutoa malalamiko na alipofika aliwakuta wote wawili mama mukwe wifi
yake akaanza kumuuliza kwanini anamtukuna kisa yeye hazai ndipo
Elizabeth akajibu nilikuwa nakutafuta siku nyingi kisha akamshuka
mtoto akamkabidhi mama yake kumvaa Vaileth’ alisema Kyola baba mzazi wa
Vaileth
Wakati
ugomvi huo unaendelea na mama Mukwe akishudia bila kuchukua hatua
Elizabeth alionekana kuwa na nguzu hivyo alimuangusha Vaileth chini na
kuchukua maji yaliyo kuwa yanachemshwa motoni kwa ajili ya kupikia
akamgwajia na kumuunguza mgongo na matakoni.
‘Mimi
nimepewa taarifa na rafiki yake ambaye aliongiozana naye wakati
wakienda kwa wakwe na nilipofika tulikuta amesha unguzwa tukampa huduma
ya kwanza kwa kupaka asali lakini baadaye tulimempeleka katika Zahanati
ya Bakwata ya Kiwila ambapo alitibiwa na nyumba nyumbani tunaendlea
kumuuguzi’ alisema Kyola.
Mwaandishi
wa habari hizi alimtafuta mume wa Vaileth, James Mwatabela kwa njia
simu yake mkononi hakuweza kupatikana ili kuzungumzi suala hilo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhairi Kidavashari alidhibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba mtuhumiwa alishakamatwa na kupelekwa katika kituo
cha Polisi Tukuyu-Rungwe na taratibu za kumfikisha mahakamni
zinaendelea.
Post a Comment