0


Vikundi mbalimbali vilivyoudhulia mafunzo ya kuwajengea uwezo,mafunzo yaliofanyika katika ukumbi wa halmshauri ya wilaya ya Liwale (picha na Liwale Blog)

 Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Liwale mkoani Lindi ,Mary Ding’ohi akifungua mafunzo ya kuvijengea uwezo vikundi vya vijana na wanawake


Mfuko wa maendeleo ya vijana na wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi umeweza kutoa mikopo ya shilingi 39,000,000 kwa vikundi 21 vyenye sifa  kwa vijana na wanawake na vimetakiwa kutumia mkopo huo kwa shughuli za kiuchumi.

Hayo yamesemwa na mgeni rasmi afisa maendeleo ya jamii wilayani Liwale,Mary Ding’ohi wakati akifungua mafunzo ya kuvijengea uwezo vikundi vya vijana na wanawake,mafunzo yaliyofanyika januari 19 mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale.

Ding’ohi amesema mikopo hiyo hutolewa kwenye vikundi  vyenye sifa ambavyo vimeanza kuwa na shughuli ya kufanya ndipo hupewa mikopo ya kuendeleza kutoka kwenye mfuko wa maendeleo ya jamii  na ametoa wito wa kuvitaka vikundi hivyo kufanya kazi kwa bidii.

Kwa upande wake afisa jinsia wilayani hapa,Florentina Mkude amesema vikundi vinatakiwa kuwa na tabia ya kujiwekea akiba kwenye akaunti zao za vikundi ili kuweza kusaidia kutatua matatizo mbalimbali na kuweza kusaidia katika kujeresha mikopo ili kuweza kuleta tija.

Nae afisa vijana Lucy Kapinga amesema miongoni wa changamoto za vikundi vya vijana kwamba  vijana wengi wenye sifa wa kukopesheka hawajajiunga kwenye vikundi vya vijana wilayani hapa aliongeza kusema licha ya kukabiliana na changamoto hizo amejipanga kuendelea kuwashawishi vijana kujiunga kwenye vikundi ili kuweze kukopesheka na kunufaika.

Katika mafunzo hayo mgeni rasmi alivitunuku vyeti vikundi 4 vilivyofanya vizuri marejesho ya mkopo katika vyeti hivyo vilitunikiwa kikundi cha City Boys kutoka kata ya Nangando,Tuinuane kutoka kata ya Mbaya,Amani kutoka kata ya Liwale B na Nufaika kutoka kijiji cha Magereza kata ya Mangirikiti.

Katibu wa kikundi cha Nufaika kutoka kijiji cha Magereza, Sauda afred  amesema katika shughuli zao za ufugaji wa kuku walikumbana na changamoto za magonjwa mbalimbali lakini changamoto hizo zimeweza kupatiwa ufumbuzi kutoka kwa maafisa ugaji kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya jamii.

Sauda alisema mkopo wa awali waliweza kurejesha kwa wakati hivyo  mkopo huu utawasaidia kupiga hatua zaidi kwani sasa wanauzoefu wa kutosha kusimamia mradi.

Nae Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Liwale (Mvili) amesema  katika mtandao huo unafanya kazi ya ufagaji wa kuku unakabiliana na changamoto nyingi ikiwemo vijana hawana mwamko wa kuchangia lakini  licha ya changamoto  watatumia muda wa kuwashawishi vijana  kujiunga kwenye vikundi mbalimbali ili kujijengea uwezo katika kukabiliana na ukosefu wa ajila.

Mvili kwa mara ya kwanza kupata mkopo Tewelewe alisema ikiwa wao vijana watatumia elimu zao kwa kushirikiana na vijana wengi watatumia fursa hiyo ya mkopo katika kuendeleza na kuibua miradi mbalimbali na kuongeza kutoa ajili ndogo ndogo kwa vijana ifikapo juni mwaka 2017.
                          Vikundi 4 vilivyotunikiwa vyeti vya wakopaji bora 
Picha ya pamoja afisa maendeleo ya jamii aliyekaa kwenye kiti (kulia) na vikundi vya vijana na wanawake (picha na Liwale Blog)

Post a Comment

 
Top