0

Rais mpya wa Marekani, Donald Trump aanza kazi hiyo kwa kutia saini amri inayolenga kufanyia mabadiliko ya mfumo wa afya ulioasiliwa na mtangaulizi wake, Barack Obama.

Hatua hiyo inataka wakala mbalimbali kupunguza mzigo wa kiuchumi wa sheria unaotokana na mfumo wa afya unaojulikana kama Obamacare.

Katika hotuba yake ya uzinduzi Ijumaa mara baada ya kuapishwa kuwa Rais aliahidi kutoa kipaumbele katika utendaji wake ‘’kwa kuitanguliza Amerika kwanza’’ na kumaliza kile alichokiita ‘’ Mauaji ya Amerika’’ ya kutelekeza viwanda na uwepo uhalifu mkubwa.

Baadaye watu wapatao 200,000 walitarajiwa kujiunga katika maandamano ya wanawake jijini Washington.

Waandaaji wa maandamano hayo wanasema wanataka kutoa msisitizo juu ya uwepo wa ubaguzi wa rangi na kukosekana kwa usawa wa kijinsia na mambo mengine ambayo yanayoonekana kuwa hatarini kukiukwa na utawala wa Trump.

Maandamano kama hayo tayari yanafanyika Australia na New Zealand na maeneo mengine mengi yanayoandaliwa katika nchi mbalimbali duniani.

Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Washington, Barbara Plett-Usher anasema Rais Trump ameapa kufanya kinachowezekana mara moja kwa kutumia madaraka aliyonayo kusukuma uhai viwanda kabla ya kurejea kuandaa muswada wa kupeleka bungeni.

Timu yake kwa haraka ilibadilisha mfumo wa wavuti wa Ikulu ya Marekani, White House,ukihusisha nia yake kuzuia mkakati wa Obama kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. Muda mfupi baada ya kushika madaraka kama rais wa 45 wa Marekani, Trump asiwasilisha mapendekezo ya baraza lake la mawaziri kwenye Seneti.

Post a Comment

 
Top