SERIKALI wilayani Handeni imezindua mradi wa kudhibiti vitendo vya
ukeketaji ujulikanao kwa jina la Kijana wa Leo “STOP FGM” (ELIMISHA) kwa
watoto na wanawake.
Mradi huo umeandaliwa na AMREF shirika lisilo la kiserikali,umezinduliwa Wilayani Handeni katika ukumbi wa Kanisa la KKKT na Mkuu wa Wilaya ya Handeni , Godwin Gondwe.
Kuzinduliwa kwa mradi huo umekuja kufuatiwa kuwepo kwa jamii nyingi za wafugaji na jamii nyingine za kawaida zinazodumisha mila potofu ya ukeketaji wa watoto na wanawake bila kutambua athari wanazokumbana nazo walengwa.
Tathmini iliyofanyika imeonesha asilimia 70 ya wafugaji wanafanya ukeketaji na asilimia 30 ni jamii ya kawaida ambayo inadumisha mila hizo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Gondwe alisema kuwa jamii hazikatazwi kudumisha mila na kufanya sherehe za kimila, lakini serikali na jamii kwa ujumla haitakuwa tayari kuona tamaduni potofu kama ya ukeketaji inaendelea kukumbatiwa na kuathiri watoto na wanawake wa Wilaya ya Handeni.
Alifafanua kuwa vitendo vya ukeketaji vinamuathiri mtoto kisaikolojia ,kiafya, kiuchumi na Kielimu, hali inayopelekea utoro uliokithiri shuleni na watoto wengi kutomaliza shule na kuolewa katika umri mdogo , kutokana na mazingira wanayojengewa na mangariba wakiwa kwenye sherehe hizo za kiutamaduni.
Gondwe aliwataka wananchi kuumilikia mradi huo wa AMREF ili kila mtoto awe na haki ya kuishi na kupata haki zake za msingi ikiwemo elimu kama mtoto mwingine na kwamba jamii nzima ya Handeni iungane na kutoa ushirikiano kuanzia ngazi ya vitongoji hadi Halmashauri kwa shirika la AMREF kuondokana na vitendo hivyo kutoka asilimia 14 iliyopo sasa hadi asilimia sifuri.
Akielezea muundo mzima wa mradi huo, Meneja wa Mradi, Dk Aisha Bianaku alisema kuwa, mradi huo wameamua kuuleta Handeni baada ya kufanya tathmini na kuona kwamba katika mkoa wa Tanga ikitoka wilaya ya Kilindi, Handeni ni wilaya inayofuata kwa kushiriki vitendo hivyo vya ukeketaji. Mradi huu umedhaminiwa Sternstunden chini ya shirika la AMREF GERMAN.
Kata zitakazonufaika na mradi huu kutokana na tathimini ya uwepo wa jamii ya wafugaji wengi na kukithiri kwa tamaduni hii ya ukeketaji ni pamoja na Segera, Malezi, Konje, Kwamagome na Ndolwa.

Post a Comment