Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kuimarika kwa upatikanaji wa dawa nchini. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Idara Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa. |
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI
wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu amesema hali ya upatikanaji
wa dawa kwasasa imeboreshwa kutoka asilimia 54 iliyokuwepo mwaka jana,
hadi kufikia asilimia 74 hivi sasa.
Ameuhakikishia umma uwa upatikanaji wa dawa utaimarika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu hadi kufikia asilimia 90.
Amesema kwa sasa kati ya aina za dawa muhimu 135 zinazohitajika kuwepo MSD dawa aina 100 zinapatika kwenye maghala ya MSD
Mkurugenzi
wa MSD, Bwanakunu ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari, Dar es
Salaam leo Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo, alipokuwa kwenye mkutano
ulioandaliwa na idara katika jukumu lake la kutoa nafasi kwa Idara na
Taasisi za serikali kuelezea utekelezaji wa majukumu yao.
Katika
hatua nyingine, Bwanakunu ameeleza kuwa, MSD imefanikiwa kurejesha
Maghala iliyokuwa imekodi kwa ajili ya kuhifadhia vifaa tiba, hatua
ambayo inaokoa sh.Bilioni 4 ambazo zilikuwa zikilipwa kama kodi kila
mwaka.
Ameongeza
kuwa, tayari wamekabidhiwa kiwanja eneo la Luguruni, wilayani Ubungo
walichopewa na Rais John Magufuli ambacho kitatumika kujenga ofisi za
Kanda ya Dar es Salaam.
Kuhusu
maduka, ameeleza kuwa wiki ijayo wanatarajia kuzindua duka la dawa la
MSD mkoani Katavi, ambalo litaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka Saba,
mengine yakiwa mkoani Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Lindi, Geita
naMbeya.
Akijibu
swali juu ya ukosefu wa vifaa vyakujifungulia wajawazito Mkurugenzi
Mkuu amesema vipo vyakutosha,na zabuni ya manunuzi ya vifungashio kwa
ajili ya vifaa hivyo vyakujifungulia iko katika mchakato wa kumpata
mshitiri.
Ameeleza
kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu anaangalia namna ya kuwawezesha akina mama wasio kuwa na uwezo
wakununua vifaa hivyo ambapo
utaratibu huo atautoa baadae.
Kwa
sasa MSD inanunua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa
wazalishaji, ilikuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
unakuwaendelevu na kupunguza gharama za ununuzi wa dawa hizo, ambazo
asilimia 80 zinatoka nje ya nchi.
Post a Comment