Mbunge
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi mashuka kwenye moja
ya Zahanati ilikuwa na upungufu wa mashuka katika kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake ya kukagua na kugundua changamoto za zahanati za jimbo la mafinga mjini
Mbunge
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi kushoto akiwa na katibu wake
pamoja na mfanyakazi wa zahanati matanana wakati wa ziara yake
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwasalimia wananchi wa kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake
Mbunge
wa mafinga mjini akitandika moja ya shuka kati ya mashuka aliyoyagawa
katika zahanati mbalimbali katika jimbo lake ,Mashuka hayo yametolewa na
mfuko wa bima ya afya NHIF
Na fredy mgunda,Iringa
Mbunge
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ametoa jumla ya mashuka mia moja
(100) kwenye zahanati,vituo vya afya na hospitali ya mafinga kwa lengo
la kuboresha huduma za kiafya kwa wananchi wanaopata huduma katika
maeneo hayo.
Akizungumza
na blog hii mbunge huyo alisema kuwa aliomba mashuka kutoka mfuko wa
taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa lengo la kuboresha huduma za kiafya
katika jimbo la mafinga mjini.
“Zahanati
na vituo vya afya vingi vinachangamoto nyingi lakini moja wapo ni
kukosekana kwa mashuka ya kutosha kwenye maeneo mbalimbali ya kiafya
hivyo nilichukua jukumu la kwenda mfuko wa taifa wa bima ya afya
(NHIF)kuomba msaada wa mashuka na namshukuru mungu wamenisaidia na
kunipa mashuka haya yote”. Alisema Chumi
Aidha
Chumi aliwataka watendaji wa sekta ya afya katika jimbo la mafinga
kuwahudumia wagonjwa kwa weledi wao ili kuifanya kada hiyo kuondokana na
changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba mara kwa mara kutoka kwa
wananchi.
“Nimeleta
mashuka haya naomba mtumie na kuyatunza ili yaweze kudumu kwa muda
mrefu kwa kuwa ni mashuka yenye ubora wa hali ya juu kama mnavyoyaona
lakini boresheni huduma kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi hapo ndio
wananchi watafurahia serikali yao”.Alisema Chumi
Chumi
aliwashukuru mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa kuwapa mashuka
hayo ambayo yamefanikiwa kutatua changamoto ya ukosefu wa mashuka katika
jimbo la mafinga na amewaomba wazidi kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo.
Kwa
upande wao viongozi wa zahanati hizo walimshukuru mbunge wa jimbo hilo
Cosato Chumi kwa kujituma na kutafuta njia za kutatua changamoto kwenye
zahati zote za jimbo la Mafinga mjini tofauti na ilivyokuwa hapo awali
kwa viongozi wengine.
“Unaona
toka ameingia madarakani amekuwa akiwaleta viongozi mbalimbali wa
serikali ili kutafuta njia za kutatua changamoto za huduma za
afya,alimleta naibu waziri wa wizara ya afya na maendeleo ya jamii Hamis
Kigwangala na wengine wengi kwenye sekta nyingine”. Walisema viongozi
hao
Baadhi
ya madiwani waliendelea kujivunia juhudi za mbunge wao kwa kazi kubwa
anayoifanya kuwaletea maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini ambapo
hapo awali ilikuwa vigumu kushudia mbunge akijituma kama anavyofanya
Cosato Chumi
Naye
mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga amesema kuwa
changamoto ya huduma ya afya katika vijiji vya jimbo la Mafinga ni mbaya
na inahitaji juhudi binafsi kuwasaidia wananchi na kuongeza kuwa tatizo
la umeme ni kubwa katika vijiji ambavyo havipokupata umeme wa REA awamu
ya kwanza na pili na ndio sababu inayosababisha huduma za kiafya
kudorola katika baadhi ya vijiji.
Post a Comment