Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA)
imetangaza bei mpya za nishati ya mafuta zitakazoanza kutumika leo
Jumatano huku bei ya mafuta ya taa na dizeli ikiwa imeshuka kwa wastani
wa shilingi 66 kwa lita.
Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix
Ngamlagosi inaonesha kuwa kwa wastani kumekuwa na ongezeko dogo sana la
bei ya mafuta ya petroli ambayo kwa jiji la Dar es Salaam bado itauzwa
kwa bei ile ile ilivyokuwa mwezi uliopita.
Hata hivyo, taarifa hiyo imetoa ruhusa kwa wauzaji wa jumla na rejareja
wa mafuta nchini kuuza bidhaa hiyo kwa bei ndogo chini ya bei elekezi
iliyotangazwa na mamlaka hiyo kama njia ya kuchochea ushindani baina ya
wauzaji wa mafuta nchini.
Post a Comment