WAKAZI
wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa
chakula, ambapo sasa bei ya mahindi imepanda. Bei hiyo imetoka sh 14,500
kwa debe moja la mahindi hadi sh 20,000, mtama sh 10,000 hadi sh
17,500, udaga umetoka sh 12,500 hadi sh 17,500 huku ulezi ukifikia sh
30,000 kwa debe.
Gazeti
la habari leo limeripoti hayo katika uchunguzi wake maeneo mbalimbali
pamoja na kwenye masoko wilayani hapa. Bei hiyo imependa kuanzia Agosti
na Septemba mwaka jana na haijashuka hadi sasa.
Baadhi
ya wafanyabiashara wa nafaka kwenye soko kuu la mjini Bunda, katika
jimbo la Bunda mjini na kwenye soko la mji mdogo wa Kibara, katika jimbo
la Mwibara, walisema kwa nyakati tofauti kuwa, bei ya chakula imepanda
kutokana na kuwepo upungufu mkubwa wa chakula katika maeneo hayo.
Walisema
kuwa hali hiyo imetokana na mvua kutokunesha wilayani hapa kwa kipindi
kirefu na kusababisha mazao yaliyokuwa yamelimwa mashambani kukauka na
pia wakulima wengine kushindwa kulima kwa sababu yakuwepo ukame huo.
Walisema
kuwa wamekuwa wakiuza chakula hicho wanachokipata kutoka katika mikoa
jirani kwa bei kubwa na kwamba wao pia ulazimika kukiuza kwa bei hiyo
ili waweze kurudisha mtaji wao pamoja na faida kidogo tu.
Mfanyabiashara
katika soko kuu la Bunda, Esta Samson, alisema kuwa kwa ujumla hali ya
chakula katika wilaya inahitaji tahadhari na kwamba hata biashara yao
haiendi kama iwalivyokuwa wanatarajia.
“Hali
ya chakula katika hili soko letu ni mbaya maana kimepanda sana kutokana
na sisi tunavyouziwa kwa bei ya juu sana. Na hii hali tuseme imeaanza
mwezi wa nane na wa tisa mwaka jana. Sasa hivi gunia moja la mahindi
tunalinunua kati ya sh 110,000 hadi sh 120,000,” alisema Samson.
Baadhi
ya wananchi walisema kuwa wanakabiliwa na njaa kubwa na kwamba hali
hiyo inatokana na ukame na pia baadhi ya mazao yao yaliyokuwa shambani
yalishambuliwa na wanyama, wakiwemo tembo kutoka katika Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti.
Post a Comment