Baraza la Habari
nchini Tanzania limewasilisha kesi mahakamani kupinga Sheria ya Huduma
za Vyombo vya Habari iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo Novemba mwaka
jana.
Baraza hilo limewasilisha kesi hiyo katika Mahakama ya
Afrika Mashariki (EACJ) likishirikiana na mashirika mawili ya kutetea
haki za kibinadamu; Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.
Baraza hilo linaaka baadhi ya vifungu vya sheria, ambavyo wanasema vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza vifutwe.
Wanasema
vinakiuka matakwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zinataka nchi
wanachama kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba wa kuundwa kwa
jumuiya hiyo.
"Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unahimiza umuhimu wa
kufuata kanuni za utawala bora, utawala wa kidemokrasia, utawala wa
sheria, uwajibikaji, uwazi, haki kwa wote, usawa wa kijinsia na
kuheshimu haki za binadamu," baraza hilo linasema kupitia taarifa
iliyotiwa saini na katibu mtendaji Kajudi Mukajanga.
"Tanzania inatakiwa kuchukua hatua za kuhakikisha haki zote zilizotajwa katika mkataba huo zinafuatwa na kutekelezwa."
CHANZO:BBC
Post a Comment