0
Azam fc ya Dar es Salaam imelazimiswa sare  ya bila kufungana na    timu ya Jamhuri kutokea kisiwani katika mwendelezo wa kombe la mapinduzi linaloendelea kutimua vumbi katika uwanja mmoja wa Amani  visiqwani Zanzibar

 Mchezo huo uliorindima majira ya saa 2:30 za Usiku Azam fc  walipewa nafasi kubwa ya kupata ushindi katika mchezo huo kutokana na Jamhuri kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa mabao 6-0  dhidi ya Dar es Salaam Young African na kuonekana ni timu zaifu kutoka na makosa mbali mbali yalionekana katika mchezo huo ikiwemo safu ya ulinzi,viungo na ushambuliaji
Licha ya azam kucheza vizuri muda wote hasa katika eneo la kiungo lakini safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na nahodha John Rarael Boko ilionekana kutokua imara muda mote kutokana na kukosa kufunga nafasi Za wazi walizokuwa wanazipata
Kutokana na matokeo hayo azam wanaendelea kuketi katika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi B huku Yanga ikiendelea kuongoza kundi hilo ikiwa na point 6 na magoli 8


Post a Comment

 
Top