0
Zaidi ya wakazi 1500 wa kijiji cha Kewanja wanaoishi jirani na mgodi wa dhahabu wa ACACIA North Mara wilayani Tarime mkoani Mara wamepigwa mabomu ya machozi, kumwagiwa maji ya kuwasha na vipigo baada ya kusimamisha shughuli za mgodi huo kwa zaidi ya saa tatu kwa lengo la kushinikiza mgodi huo kuwalipa fidia ya nyumba zao 216 zilizofanyiwa tathimini tangu mwaka 2012.

Hali hiyo ya kumwagiwa maji ya kuwasha, kupigwa mabomu ya machozi na vipigo haikuwafanya wananchi hao waliokuwa wamebeba mabango kurudi nyuma.

Katibu tawala wa wilaya ya Tarime John Marwa ambaye amefika eneo la tukio kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo na kushuhudia wakazi hao wakipambana na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia, amewaomba kuwa watulivu kwani suala lao linaelekea kupatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya kipolisi Nyamongo Moris Okinda akizungumza na wananchi hao amewataka kuzingatia falsafa ya utii wa sheria bila shuruti.

Post a Comment

 
Top