Utafiti ya viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Malaria kwa mwaka
2011/2012 inaonesha maambukizi ya VVU kwa upande wa Tanzania Bara yapo
kwa asilimia 5.3.
Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ikiwa leo Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe mosi Desemba.
Amesema wanawake ndiyo wameathirika zaidi na janga hili ikilinganishwa na wanaume ambapo asilimia 6.2 ni wanawake na asilimia 3.8 ni wanaume.
Amesema pia inakadiriwa kuwa kuna watu 1,538,382 wanaishi na VVU nchini Tanzania ambapo vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni asilimia 11.8 ya watu wanaoishi na VVU nchini.
Wakati huo huo Waziri Mhagama amesema serikali inazindua mfuko wa udhamini wa Ukimwi pamoja na bodi yake lengo likiwa ni kuondoa utegemezi wa misaada kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema serikali na jamii kwa ujumla haina budi kufanya jitihada za makusudi katika kutokomeza maambukizi ya VVU na Ukimwi.

Post a Comment