wadau wa elimu wilayani Kilwa mkoani Lindi
Mwaandishi wetu
Wadau wa Elimu wilaya Kilwa wameelezwa kuwa Kushuka
kwa kiwango cha elimu wilayani kilwa humo kunachangiwa na
wazazi kutotambua umuhimu wa elimu na kusababisha kushidwa kushiriki mikakati
ya kutatua cahnagmoto za elimu wilayani humo
Hayo
yamebainishwa na wadau wa elimu wilayani kilwa wakati wa kikao cha kujadili
changamoto za uhamasishaji wa elimu bora kwa kutumia rasilimali za ndani
Wakitoa ushauri
wao wajumbe wa kikao hicho wakiwemo wenyeviti wa kamati za shule watendaji kata
madiwani na maafisa elimu kata wamesema changamoto kubwa inayosabaisha kushuka
kwa elimu wilayani humo ni wazazi kutoshiriki kikamilifu katika maswala ya
elimu
Mradi wa
uhamasishaji wa utoaji elimu bora kwa kutumia rasilimali za ndani unaotekelezwa
na action aid kwa kushirikiana na mtandao wa elimu tanzania unatekelezwa katika
wilaya mbili za kilwa na singida vijijini.
Post a Comment